info@ngomesaccos.co.tz
: +255(0) 739 999 797
Sehemu hii inaeleza muumuundo wa chama unaojumuisha Mkutano Mkuu, Bodi ya Chama, Kamati mbali mbali, Meneja, Idara na vitengo vyake kama itavyofafanuliwa kwenye sera ya utumishi. Vilevile, kwa kipindi cha miaka mitano chama kinaweza kuongeza watendaji kwa siku zijazo ili kutekeleza mikakati ya Chama kwa wakati.
Hiki ndicho chombo kikuu cha maamuzi katika Chama. Wajibu wa mkutano mkuu umeelezwa na Masharti ya Chama katika shemu ya Tisa.
Hiki ndicho chombo kikuu cha usimamizi wa shughuli zote za chama ambacho huchaguliwa na wanachama katika mkutano mkuu wa chama. Kazi za Bodi ya Chama zimeelezwa katika Masharti ya chama sehemu ya Kumi.
Kamati hii itakuwa na wajumbe watatu ambao wamechaguliwa na Wanachama kwa ajili ya kuhakikisha kuwa,taratibu za uendeshwaji wa chama unazingatia Sheria ya Vyama vya ushirika Na. 06 ya mwaka 2013 na Masharti ya chama pamoja na miongozo mingine. Kazi za kamati ya Usimamizi zimeelezwa katika Masharti ya Chama katika kifungu cha 55.
Kamati hii itakuwa na wajumbe watatu ambao huchaguliwa miongoni mwa wajumbe Bodi. Kazi kuu ya kamati ya mikopo ni kusimamia utaratibu wa utoaji, ufuatiliaji na kuishauri Bodi juu ya ufugaji wa mikopo mibaya kwa kuzingatia Sera ya Mikopo ya Chama.
Kutakuwa na kamati ya uwekezaji inayosimamia mawekezo yote ya chama.
Huyu ni mtendaji ambaye ameajiriwa na Bodi ya chama kwa ajili ya kusimamia maswala maziama ya kifedha. Moja ya kazi muhimu ya Meneja Fedhani:-
1. Kuandaa na kutekeleza sera na taratibu fedha na uhasibu.
2. Kuaandaa taarifa zote za fedha za kila mwezi, kila Robo mwaka na kwa kila mwaka.
3. Kazi nyinginezo kwa mujibu wa maelekezo ya Bodi ya chama na kanuni za utumishi za chama.
Mkaguzi wa ndani atakuwa na jukumu la kuhakikisha kuna uthibiti bora wa mifumo ya ndani pamoja na majukumu mengine kama yalivoainishwa katika kanuni ya 56 ya huduma ndogo za fedha ya mwaka 2019.
P.O.BOX 35923 , Mwenge,Dar es Salaam, Tanzania
info@ngomesaccos.co.tz
+255(0) 222 923 862
+255(0) 739 999 797
+255(0) 739 999 797
+255(0) 222 923 861
Developed by: Ponsi Kihaga
Contact: poncekihaga@gmail.com.