info@ngomesaccos.co.tz
: +255(0) 739 999 797
Wanachama wake ni "Maafisa, Maaskari, Wastaafu pamoja na watumishi wa Umma wa Wizara ya ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa na wale waliohamia wizara nyingine wakiwa wanachama Hai wa Ngome SACCOS.
Wasiliana nasiKuwa SACCOS bora yenye kutoa riba nafuu inayoongoza kwenye utoaji wa huduma za kifedha kitaifa na kimataifa
Kukusanya akiba kwa ajili ya kuwakopesha wanachama kwa riba nafuu na kuwaelimisha namna ya kutumia mikopo hiyo kwa busara ya kuwajengea uwezo mkubwa wa kiuchumi na maisha bora.
Misingi ni suala la muhimu wakati wa kusimamia shughuli za chama kwani husaidia kufikia malengo ya chama kwa wakati.
Chama kitazingatia maadili yafuatayo wakati wa kutekeleza shughuli zake:-
Mafanikio ya chama yatafikiwa endapo kutakuwepo na ushirikiano na mshikamo wa karibu kati ya wanachama, Bodi watendaji na wadau wengine. Ni wajibu wa kila mdau kutoa Ushirikiano pale inapohitajika kufanya hivyo.
Viongozi wa chama, Wanachama na watendaji wanapaswa kuwajibika kwa masilahi mapana ya Chama.
Mara zote Viongozi wa chama pamoja na watendaji watapaswa kutoa huduma iliyo bora kwa wanachama wake.
Shughuli za chama zitaendeshwa katika hali ya uwazi kwa kuzingatia misingi ya kumlinda mwanachama (Consumer protection) pamoja na kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya chama.
Bodi pamoja na watendaji watapaswa kuzingatia na kufuata viwango vya kitaalamu walivyonavyo wakati wa kuendesha shughuli za chama.
Viongozi wa chama pamoja na watendaji wanapaswa kuwa waaminifu wakati wa kuendesha shughuli za chama.
Viongozi wa chama na watendaji wanahamasishwa kuwa na moyo wa kujitolea na kujitegemea wakati wote kwa manufaa ya chama na wanachama wake.
Viongozi wanachama na watendaji wanapaswa kuwa waadilifu muda wote.
Huduma za chama zitatolewakwa misingi ya uwasa.
Viongozi watatakiwa kutotoa taarifa za chama bila idhini.
P.O.BOX 35923 , Mwenge,Dar es Salaam, Tanzania
info@ngomesaccos.co.tz
+255(0) 222 923 862
+255(0) 739 999 797
+255(0) 739 999 797
+255(0) 222 923 861
Developed by: Ponsi Kihaga
Contact: poncekihaga@gmail.com.