info@ngomesaccos.co.tz

:  +255(0) 739 999 797

Machapisho

Nyumbani | Habari
Habari Mpya

Tangazo la Mkutano Mkuu wa 19 Mwaka 2024 wa NGOME SACCOS Ltd

   Bodi ya NGOME SACCOS Ltd inawatangazia Wawakilishi wa Wanachama kuwa, Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 19 utafanyika Jijini Dar es salaam tarehe 01 Nov 2024 kwenye Ukumbi wa 302 KV Brigade Mess kuanzia saa 2:00 asubuhi. Wawakilishi wa Wanachama wanatakiwa kuhudhuria kwenye Mkutano huo.

   Wawakilishi watatakiwa kuthibitisha ushiriki/kutoshiriki kwa barua au barua pepe info@ngomesaccos.co.tz au kwa simu namba 0739999797/98,   Fax namba 0222923861.

AGENDA

1.       Kuhakiki Akidi ya Mkutano Mkuu.

2.       Kuchagua Mwenyekiti wa kuongoza Mkutano Mkuu.

3.       Kufungua Mkutano Mkuu.

4.       Kupitia na kuhakiki Agenda za Mkutano.

5.       Kufuta wanachama, kuridhia na kuwakaribisha Wanachama wapya.

6.       Kusoma muhtsari wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Mwaka 2023.

7.       Kuidhinisha muhtasari wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Mwaka 2023.

8.       Yatokanayo na muhtasari wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Mwaka 2023.

9.       Kuidhinisha maboresho ya sera.

10.      Kuwasilisha na kujadili taarifa ya Meneja Mkuu.

11.      Kuwasilisha na kujadili taarifa ya Mwakilishi Mkuu.

12.      Kuwasilisha na kujadili taarifa ya Kamati ya Usimamizi.

13.      Kuwasilisha taarifa ya Mwenyekiti wa Bodi.

14.      Kusoma na kujadili taarifa ya hesabu zilizokaguliwa na Mkaguzi wa Nje.

15.      Kupitia na kujadili maombi ya kufutwa madeni mabaya.

16.      Kujadili na kupitisha makisio ya mapato na matumizi ya kawaida.

17.      Kusoma na kupitisha makisio ya mapato na matumizi ya maendeleo.

18.      Kuwasilisha, kujadili na kupitisha mapendekezo ya kuongeza Mtaji na Ukwasi.

19.      Kusoma na kupitisha maombi ya ukomo wa madeni.

20.      Kujadili na kupitisha Mkaguzi wa Nje.

21.      Uchaguzi wa Viongozi.

22.      Kufunga Mkutano.

“USHIRIKA HULETA WATU MAKINI PAMOJA”

 

(Aisha O. Matanza, ndc)

Kanali

Mwenyekiti wa Bodi

Anwani

P.O.BOX 35923 , Mwenge,Dar es Salaam, Tanzania

info@ngomesaccos.co.tz

+255(0) 222 923 862

+255(0) 739 999 797

+255(0) 739 999 797

+255(0) 222 923 861

Follow Us

Kikokotozi Cha Mikopo

Developed by: Ponsi Kihaga  


Contact:   poncekihaga@gmail.com.