NGOME SACCOS ni ushirika wa akiba na mikopo unaoundwa na maafisa, askari, watumishi wa umma na wastaafu toka wizara ya Ulinzi na jeshi la kujenga Taifa, ambao ulisajiliwa tarehe 30 April 2007 kama asasi ya kati ya huduma za kifedha chini ya sheria ya vyama vya ushirika namba 20 ya mwaka 2003.

Tovuti hii ni mahsusi kwa ajili yako mwanachama au unayetaka kuwa mwanachama wetu kuweza kupata taarifa mbalimbali zinazohusu ushirika wetu, pia kukupa njia rahisi ya mawasiliano. Ni matumainiyetu kuwa utapata kufaidi na kujifunza mengi kuhusu ushirika wetu ukiwa hapa. Karibu sana.