Have a question?

MIKOPO YETU NA AINA ZAKE

AINA ZA MIKOPO

1 MIKOPO YA DHARURA

Mikopo hii itatolewa kwa mwanachama kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya dharura/ulazima kwa mwanachama. Mwanachama atajaza fomu ya maombi ikionesha kiasi cha mkopo na muda wa marejesho. Kiwango cha juu cha mkopo hakitazidi shilingi milioni moja na muda wa marejesho hautazidi miezi kumi na mbili. Dhamana ya mkopo itakuwa akiba alizonazo mwanachama na riba itakuwa asilimia ishirini (20%) kwa mwaka mmoja.

Mkopo huu hutolewa kipindi chochote ili mradi pawepo na fedha katika chama/tawi. Afisa mikopo ataidhinisha mkopo na meneja atatoa taarifa kwenye kikao cha bodi kitakachofuata. Mwanachama anaweza kukopa mkopo wa dharura hata kama ana mkopo mwingine kama salio la mshahara linaruhusu kukatwa ndani ya miezi kumi na mbili. Mkopo huu hutolewa ndani ya masaa inshirini na nne (24) ya kazi. Adhabu ya kuhuni (kutorejesha) rejesho lolote itakuwa asilimia kumi (10%) ya mkopo wote.
emegenc copy

2 MIKOPO YA MAENDELEO

Mikopo hii hutolewa kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya muda mrefu ya mwanachama. Kiwango cha mkopo ni mara tatu ya akiba za mwanachama ambazo zipo katika akaunti yake kwa miezi mitatu iliyopita na hazikuwekwa kwa mkupuo, muda wa marejesho hautazidi miaka mitatu (3). Mkopo huu unaweza kulipwa kwa kutumia mshahara au fedha taslimu toka kwenye biashara husika.

Kiwango cha riba kitategemeana na soka la fedha kwa wakati husika (kwa sasa riba ni asilimia kumi -10%) kwa mwaka kwa njia nyoofu. Mikopo hii ni kutokana na fadha za ndani na riba yake itakuwa pungufu kulingana na mikopo ya uwiano wa mshahara. Mwombaji lazima ajaze fomu ya maombi itakayoidhinishwa na mkuu wa kikosi au wa idaya ya mkopaji.

Maombi ya mkopo yafikishwe chamani kabla ya tarehe thelathini (30) ya kila mwezi na mkopo utalipwa tarehe kumi (10) ya mwezi unaofuata. Mkopaji anaweza kuongezewa mkopo ikiwa marejesho yake yamefikia zaidi ya nusu ya mkopo aliochukua na mshahara unaruhusu makato. Mwanachama atatayarisha mchanganuo wa biashara na kujaza mkataba wa mkopo ambao utadhibitishwa na mwanasheria au hakimu wa mahakama.

 

Dhamana ya Mkopo wa Maendeleo:

Mkopo wa chini ya milioni tano (5,000,000/=) utadhaminiwa na akiba za mwanachama na wadhamini wawili. Mkpo zaidi ya uwezo wa marejesho kwa mshahara utadhaminiwa na akiba na akiba za mkopaji na mali zisizohamishika zenye thamani zaidi (kwa asilimia ihsirini – 20%). Uongozi wa chama lazima uridhie kuwa mali iliyotolewa inawezekana kisheria kumilikiwa kwa pamoja kati ya cham na mwanachama mpaka marejesho ya mkopo na riba yatakapokamilika.

Mali iliyowekwa dhamana dhamana itarejeshwa kwa mwanachama mara tu baada ya mkopo wake na riba kulipwa kwa kikamilifu. Endapo mkopajiatashindwa kulipa deni lake katika muda uliopangwa na baada ya juhudi za makusudi kushindikana, chama kitachukua akiba zake na kuuza dhamana hiyo ili kufidia deni husika

3MKOPO WA USTAWI [DOMESTIC/PERSONAL LOAN

Kiwango cha mkopo kitatokana na mshahara wa mwanachama na muda wa marejesho haitazidi miezi thelathini na sita (36) au muda usliosalia wa mwanachama kustaafu. Kiwango cha juu cha kukatwa kwenye mshahara kitakuwa 2/3 ya mshahara wa mwanachama (Net Pay) ila net salary isipungue 1/3 ya gross pay.
Kiwango cha juu cha mkopo hakitazidi ¼ ya mafao ya ajira yatakayotarajiwa na mkopaji. Riba itategemea soko la fedha la wakati husika ila kwa sasa ni asilimia kumi na tatu (13%)kwa mwaka kwa mkopo wa njena asilimia kumi (10%) kwa mkopo wa ndani. Mwanachama ataambatanisha salary slip ya miezi miwili (2) ya karibuni pamoja na fomu za maombi.

4 MKOPO WA ELIMU

Mkopo huu utatolewa kwa wanachama na familia yake ya karibu (nuclear family), muda wa mkopo huu ni mwaka mmoja. Kiwango cha mkopo kinategemea na Ankara kutoka katika shule au chuo lakini hakitazidi milioni tatu na riba ya mkopo huu ni asilimia kumi na tano (15%) kwa mwaka. Mkopo utalipwa moja kwa moja kwenye shule au chuo kinachohitajika kulipiwa.

student

5 MKOPO WA MAFAO YA KUSTAAFU

Mkopo huu hutolewa kwa wanachama waliobakiza miezi sita (6) au zaidi kustaafu. Ni maalumu kwa kukidhi mahitaji ya ulazima ya mwanachama anayetarajia kustaafu – mfano kumalizia ujenzi. Kiwango cha mkopo ni kuanzia milioni kumi (10) na kitategemea na mshahara wa mwombaji.

Mkopo huu utaanzwa kurejeshwa kwenye miezu iliyobakia ya utumishi na bakaa ya mkopo kulipwa toka katika mafao ya mkopaji. Muda wa mkopo utategemea muda uliobakia mwanachama kustaafu lakini hautazidi miezi sista (6).

6 MKOPO WA TAHADHARI

Mkopo huu hutolewa kwa wanachama wenye mahitaji ya kulipia bima za mali zao, muda wa mkopo ni mwaka mmoja tu.kiwango cha mkopo kitategemeana na madai ya bima anayodaiwa au kutakiwa kulipa lakini hakitazidi shilingi milioni moja.

Riba ya mkopo huu ni asilimia ishirini (20%) kwa mwaka, mkopo utalipwa moja kwa moja kwa wakala au kwa mwanachama kulingana na mkubaliano. Mkopo huu utatoka ktk mfuko wa tahadhari.

7 MKOPO WA KUJIKOMBOA

Mkopo huu hutolewa kwa mwanachama mwenye mkopo uliofanyiwa marejesho kwa wakati na kufikia chini ya nusu ya deni. Mkopo utatolewa kwa kuzingatia uwezo wa mshahara wa mwanachama kurejesha na uzito wa tatizo unaomfanya komba mkopo wa ziada (Top up loan).

Mkopo hautazidi milioni kumi (10,000,000/=) kwa kuzingatia mshahara kurejesha ndani ya miaka mitatu (3). Mkopo uliopo utakatwa kutoka ktk mkopo wa nyongeza na mwanachama kupewa fedha iliyobaki. Riba ya mkopo huu ni asilimia kumi na tatu (13%) kwa mwaka na muda wa mkopo si zaidi ya miaka mitatu (3).

8 MKOPO WA MAKAZI/UJENZI

Mkopo huu utatolewa kwa mwanachama aliyeweka akiba kwenye mfuko wa makazi. Mwanachama ataweka akiba ya silimia ishirini ya tano (25%) ya mahitaji yake na kukopeshwa asilimia mia (100%) ya mahitaji yake kwa awamu kulingana na makubaliano ya hatua za ujenzi.

Mwanachama anatakiwa kuweka rehani ya mali isiyohamishika na kudhaminiwa na wanachama wawili kama mkopo atakaopewa ni zaidi ya uwezo wa mshahara wake kurejesha ndani ya miezi thelathini na sita (36). Riba ya mkopo huu ni asilimia kumi na tatu (13%) kwa mwaka na muda wa mkopo ni miezi arobaini na nane (48)

9 MKOPO WA KILIMO

Mkopo huu hutolewa kwa wanachama walioweka akiba katika mfuko wa kilimo. Mwanachama ataweka akiba ya asilimia ishirini (20%) ya mahitaji yake na kukopeshwa asilimia mia moja (100%) ya mahitaji yake kwa awamu kulingana na makubaliano ya hatua za kilimo.
Mwanachama anatakiwa kuweka rehani ya mali isyohamishikana kudhaminiwa na wanachama wawili kama mkopo wake ni zaidi ya uwezo wa mshahara wake wa kurejesha ndani ya ndani ya miezi thelathini na sita (36%). Kutakuwa na muda wa hisani kwa mkopo huu usiozidi miezi mitatu, muda huu wa hisani utalipwa riba sawa na itakayolipwa kwa mkopo huu kwa kila mwezi. Mkopo wa kilimo unajumuisha ununuzi wa pembejeo na zana za kilimo.

10 MKOPO WA GARI/USAFIRI

Mkopo huu hutolewa kwa mwanachama aliyeweka akiba kwenye mfuko wa mikopo ya magari. Mwanachama ataweka akiba yay a asilimia thelathini (30%) ya thamani ya gari na kukopeshwa asilimia mia moja (100%) ya manunuzi ya gari husika.
Mwanachama anatakiwa kuweka rehani ya gari husika kwa kusajili gari hilo kwa jina lake na la chama na kudhaminiwa na wanachama wawili mwanachama anatakiwa kukata bima kamilifu (COMPREHENSIVE INSURANCE) kwa mkopo wa tahadhari au kwa fedha zake mwenyewe na muda wa mkopo huu ni miezi thelathini na sita (36).
Riba ya mkopo ni asilimia kumi na tatu (13%) kwa mwaka, mwanachama akikamilisha marejesho ya mkopo atawajibika kubadilisha usajili wa gari kwa kuondoa jina la chama kwenye usajili.
637692094-ktIG--621x414@LiveMint

11 MKOPO WA SAMANI


Mkopo huu utatolewa kwa mwanachama aliyeweka akiba kwenye mfuko wa mikopo ya samani. Mwanachama ataweka akiba ya silimia thelathini (30%) ya gharama ya samani anayotaka kununua na kukopeshwa asilimia mia moja (100%) ya manunuzi ya samani husika.

Mwanchama anatakiwa kuweka rehani ya mali isiyohamishika na kudhaminiwa na wanachama wawili kwa mkopo zaidi ya uwezo ya marejesho ya mshahara. Mwanachama anaweza kulipiwa samani kwenye maduka ya jeshi yenye mkataba na chama wa kuwapatia samani wanachama na kulipiwa na chama au kupewa mkopo wake akanunua mwenyewe kwa kadiri atakavyokubaliana kwenye maombi. Muda wa mkopo ni miezi thelathini na sita (36%) na riba ya mkopo ni asilimia kumi na tatu (13%) kwa mwaka.

12 MKOPO WA KUPUMULIA

Mkopo huu hutolewa kwa mwanachama mwenye matatizo ya kifedha na mshahara wake kwa mwezi husika, hauna bakaa ya marejesho hata akikopeshwa. Riba ya mikopo ni asilimia ishirini na tano (25%) kwa mwaka na haina muda wa hisani, muda wa marejesho ni mwaka mmoja tu.

VIGEZO VYA KUPATA MKOPO

Mikopo hii itatolewa kwa mwanachama kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya dharura/ulazima kwa mwanachama. Mwanachama atajaza fomu ya maombi ikionesha kiasi cha mkopo na muda wa marejesho. Kiwango cha juu cha mkopo hakitazidi shilingi milioni moja na muda wa marejesho hautazidi miezi kumi na mbili. Dhamana ya mkopo itakuwa akiba alizonazo mwanachama na riba itakuwa asilimia ishirini (20%) kwa mwaka mmoja.
Mkopo huu hutolewa kipindi chochote ili mradi pawepo na fedha katika chama/tawi. Afisa mikopo ataidhinisha mkopo na meneja atatoa taarifa kwenye kikao cha bodi kitakachofuata. Mwanachama anaweza kukopa mkopo wa dharura hata kama ana mkopo mwingine kama salio la mshahara linaruhusu kukatwa ndani ya miezi kumi na mbili. Mkopo huu hutolewa ndani ya masaa inshirini na nne (24) ya kazi. Adhabu ya kuhuni (kutorejesha) rejesho lolote itakuwa asilimia kumi (10%) ya mkopo wote

JINSI YA KUPATA MKOPO

BONYEZA HAPA KAMA UNASTAHILI MKOPO